歌词
Niliamini mapene hayatoshi.na niki-hustle siyakosi/
Sababu. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
Kwahivyo nikaenda Dar na treni... of thoughts./
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
Sikutaka kuivaa mikosi.nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport.password. pin.lakini ni crack codes/
Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine.hatuko fine/
Je mimi ni kaka mubaya...? kaka aso haya./
KAKA.? huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/
Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata. makaka hamkui?
Mmeendekeza hila. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball... hata kwa mpira wa makaratasi/
Unaweza ukahisi mie napita tu. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
Ukiwa idle. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE. life ni zaidi ya ku-have fun/
Kwani. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi. huimiss tafsiri yenyewe/
Nalindwa na dua za mama. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama. yenye maana yamchukue/
Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
Ndiyo. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
Mie ni mbishi. muulize Nikki - hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba.